You are here: Home / Products Catalogue / All Products / Best Sellers / Kiswahili Mufti 2

Kiswahili Mufti 2

Email
Rating: Not Rated Yet
Price:
Sales price without tax: Ksh: 440.00
Tax amount: Ksh: 70.00
Sales price: Ksh: 510

ISBN: 9966 36 289 4

AUTHOR NAME: Wallah Bin Wallah

Description

Toleo hili la Kiswahili Mufti darasa la Pili linatimiza kikamilifu mahitaji na mada zote za silabasi mpya iliyoanza kutekelezwa shuleni kuanzia 2003. Kitabu hiki kimeandikwa kwa ungalifu mkubwa ili kiweze kueleweka vizuri zaidi na wanafunzi wote kutoka mazingira mbalimbali. Msamiati uliotumika katika vifungu vya ufahamu unaafikiana vyema zaidi na uwezo wa lugha wa wanafunzi katika kiwango hiki. Toleo hili limeshughulikia kikamilifu maswala ibuka kama vile mazingira, haki za watoto, UKIMWI na maadili. Kitabu hiki kitawaondolea wazazi gharama ya kununua vitabu vingi kwa ajili ya somo hili moja na kuwapunguzia walimu tatizo la kupekua vitabu vingi ili kutosheleza masharti ya silabasi. Vitabu vyote katika mfululizo huu vimeshughulikia silabasi kwa upana, urefu, ukamilifu na usasa unaovutia. Kila kitabu katika mfululizo huu kinaweza kutumika kwa mafundisho, marudio na marejeo kwa sababu mafunzo na mazoezi chungu nzima yaliyomo yanashughulikia sehemu zote za lugha na mazingira tofauti za maisha. Wale ambao wamekisoma Mazoezi na Marudio ya Gateway KCPE Kiswahili wanaufahamu ubingwa wa Wallah Bin Wallah. Vipengele muhimu vilivyoshughulikiwa katika kitabu hiki ni: (a) Ufahamu – hadithi za kusisimua pamoja na maswali ya ufahamu. (b) Sarufi – ngeli, umoja na wingi, vivumishi, vitenzi, vihusishi, kinyume n.k (c) Matumizi ya lugha – methali, vitendawili, tarakimu, misamiati n.k (d) Kusoma – hadithi, maneno yanayotatanisha n.k. (e) Kuandika – hati nadhifu, hatiwima, hatimlazo n.k (f) Mtungo – mazungumzo na maelezo mafupi. (g) Mazoezi – mazoezi mengi yanayoshughulikia vipengele vyote vilivyofundishwa.

Reviews
There are yet no reviews for this product.

VM - Shopping cart

 x 
Cart empty